TAWASALI

TAWASALI

TAWASALI

Interpreter :

Hemedi Lubumba

Publish number :

Toleo la kwanza

Publish location :

Dar es Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

TAWASALI

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la, at-Tawassul. Sisi tumekiita, Tawasali. Kitabu hiki, Tawasali, ni matokea ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni wa Kiislamu, Sayyid Abdul Rahim al-Musawi. Kumekuwepo na zogo kubwa katika miji yetu ya Kiislamu kuhusu usahihi wa tawasali. Baadhi wanasema, ni sahihi kutawasali, na wengine wanasema, ni bidaa - yaani jambo lililozushwa na kuingizwa katika dini. Baadhi ya masheikh wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamu wenzao kuwa ni mushirikina au makafiri. Sheikh Muhammad bin Abdul Wahhab, amewaita mushirikina wale Waislamu wanaotawasali akisema: “Iwapo baadhi ya mushirikina [yaani Waislamu wasiokuwa Mawahabi] wakikwambieni: Sikilizeni! Hakika vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawana khofu wala hawahuzuniki; au shufaa ni haki, au Manabii wana jaha kwa Mwenyezi Mungu, au akatoa maneno ya Nabii ambayo kwayo anafanya ni dalili juu ya batili yake, na ikawa wewe hufahamu [yaani huna uwezo wa kumjibu], basi jibu lake ni kumwambia: ‘Hakika Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu Chake ametaja kuwa - ambao ndani ya nyoyo zao mna upotovu huacha aya zilizo waziwazi na hufuata yaliyofichikana.’” Sheikh Abdul Aziz bin Baaz, anasema: “Atakayemwomba Nabii na kumwomba shufaa, basi ametengua Uislamu wake.” Haya ndiyo maoni ya masheikh hawa wawili wa Kiwahabi kuhusu kutawasali na wale ambao wanaitekeleza. Lakini je, tawasali haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ni ibada maalumu na ina asili katika dini kama utakavyoona katika kitabu hiki. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeona bora ikichapishe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.