Uislamu-na-mafunzo-ya-kimalezi

Uislamu-na-mafunzo-ya-kimalezi

Uislamu-na-mafunzo-ya-kimalezi

Interpreter :

Hemedi Lubumba

Publication year :

2014

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Uislamu-na-mafunzo-ya-kimalezi

K itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, Al-Islam wa Taalimul Tarbawiyyah kilichoandikwa na Sayyid Muhammad al-Qazwini. Sisi tumekiita, Uislamu na Mafunzo ya Kimalezi.
Uislamu ni dini na ni mfumo kamili wa maisha haukuacha lolote linalomhusu mwanadamu kimwili au kiroho bila ya kuweka sharia za kuyaendesha maisha hayo (kiroho na kimwili). Katika kitabu hiki mwandishi anaelezea kwa ujumla malezi, adabu na maadili ya Kiislamu kuanzia utotoni, ujanani, utu uzimani hadi uzeeni, na kuonyesha njia nzuri za kusoma na kazi za kufanya.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kwa hiyo, Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu al-Hajj Hemedi Lubumba Selemani kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Aidha tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin