USUULID DIIN UIMAMU

USUULID DIIN UIMAMU

USUULID DIIN UIMAMU

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

USUULID DIIN UIMAMU

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote, na rehma na amani ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad na Kizazi chake Kitukufu.
"Uimamu" kwa waislamu ni miongoni mwa maudhui ambayo yamezungumzwa sana na kufanyiwa utafiti sana, hadi vitabu vilivyo tungwa kuhusu maudhui haya kufikia maelfu kwa maelfu.
Kisha yakaendelea mazungumzo kuyahusu maudhui hayo, na watafiti kugundua wingi wa kuchipuka kwa matawi yake na upana wa maudhui haya katika utungaji wa vitabu, na kwa hivyo kila kundi kati ya watunzi hao likachukuwa tawi moja wapo kati ya matawi yale au upande mmoja wapo wa maudhui hayo, na matokeo ya kufanya hivyo ukatokea upande ufanyao utafiti na kujihusisha na suala la uimamu ndani ya Qur'ani.
Na upande mwengine ukajihusisha na suala hilo kwa upande wa hadithi za Mtume, na kuna upande uliojihusisha na uimamu kwa mtizamo wa elimu ya akida, au kwa upande wa historia, au kuuangalia uimamu kwa kuzingatia mipaka ya yale yaliyo tokea kwenye Saqifa bani Saida pindi alipo fariki Mtume (s.a.w.w), kisha yaliyo husiana na maisha ya Maimamu na historia zao, na kue-ndelea.