Abu Twalib
Abu Twalib

0 Vote
47 View
Siku kama ya leo miaka 1446 iliyopita, Abu Twalib ami ya Mtume Muhammad (SAW) na baba wa Imam Ali (A.S) alifariki dunia wakati Waislamu walipokuwa chini ya mzingiro wa washirikina wa Makka. Abu Twalib alikuwa pamoja na Waislamu wengine huko katika Shiibi Abi Twalib. Mtume Muhammad (SAW) alikuwa chini ya uangalizi wa Abu Twalib tangu alipokuwa na umri wa miaka minane, baada ya kuaga dunia babu yake, Abdul Muttalib. Abu Twalib alisilimu baada ya kubaathiwa Mtume na alikuwa muungaji mkono na mtetezi mkubwa wa Mtume Mtukufu dhidi ya washirikina wa Kikureishi. Kabla ya kuiaga dunia, Abu Twalib aliwausia jamaa na marafiki zake kufuata Uislamu na kumtetea Mtume Muhammad (saw). Katika mwaka uhuo huo wa kifo cha Abu Twalib, aliaga dunia pia Bibi Khadija, mke mwaminifu na mwema wa Mtume wetu Muhammad (saw), na kutokana na ukubwa wa huzuni na masikitiko yaliyosababishwa na matukio haya mawili, Mtume aliutaja mwaka huo kuwa ni “Aam Al- Hazn", kwa maana ya mwaka wa huzuni.