Ammar Yasir _ Msahaba Mjulikana wa Mtukufu Mtume (saww)
Ammar Yasir _ Msahaba Mjulikana wa Mtukufu Mtume (saww)
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2006
Publish location :
Dar es salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Ammar Yasir _ Msahaba Mjulikana wa Mtukufu Mtume (saww)
Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la Ammar Yasir.Kitabu hiki kama kile cha Bilal wa Afrika, Abu Dhar na Salman Farsi kinahusu maisha ya Sahaba mwingine mkubwa na mashuhuri Ammar Yasir. Ammar aliukubali Uislamu na Mtume wake mwanzo kabisa pamoja na baba yake na mama yake. Mama yake aliuliwa shahidi mwanzoni kabisa mwa Uislamu, na kuwa shahidi wa kwanza kabisa katika Uislamu akifuatiwa na mume wake Yasir. Katika watu mashuhuri na masahaba wa mtume ambao wamekuwa madhulumu wa historia ya Uislamu, Ammar alikuwa mmoja katika watu hao. Na sababu yenyewe iko wazi; Ammar hakuwaunga mkono moja kwa moja Makhalifa wa wawili wa mwanzo (Abu Bakr na Umar) ingawa alishirikiana nao vizuri, lakini tatizo lilikuja kuwa kubwa wakati wa kipindi cha Khalifa wa tatu (Uthman), huyu alimpinga waziwazi na alifanya hivyo kwa nia nzuri tu ya kulinda heshima na maadili ya Uislamu. Kwa kuwa wanahistoria na waandishi wengi wa mwanzo waliandika kwa kuwaridhisha watawala wa wakati huo hususan utawala wa Bani Umayya ambao ndio ukoo anaotoka Khalifa Uthman, hawakutaka kusikia habari za mtu kama Ammar na wengine kama yeye. Mwandshi wa kitabu hiki amejitahidi kwa uwezo wake angalau kutupa picha sahihi ya Sahaba huyu Mkubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w).