Bibi fatima kiigizo chema
Bibi fatima kiigizo chema
Author :
Interpreter :
Publisher :
(0 Kura)
(0 Kura)
Bibi fatima kiigizo chema
Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni sehemu ya tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: Al-Hijab Saa'datun laa shiqaaun, kilichoandikwa na, Sheikh Muhammad Ibrahim El-Qazwiniy Kitabu hiki kinahusu vazi la Hijabu: vazi ambalo ni rasimi kwa wanawake wa kiislamu kwa ajili ya kustiri maungo yao. Katika kitabu hicho tumechukua kipengele kimoja tu, kinacho husiana na bibi Fatima (s.a) ambacho nia: Bibi Fatima (a.s) Kiigizo Chema Kwa Wanawake. Kipengele hicho tumekinyambua kutoka katika kitabu hicho kwa mnasaba wa masiku ya Shahada ya Bibi huyo mtukufu, kwa lengo la kumuenzi Mama huyo Adhimu. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa kwa wasomaji wetu, hususan wanawake wa kiislamu na kuiokoa jamii yetu kutokana na maovu. Pia Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Msabah S. Mapinda kwa kukubali kwake kuchukuwa jukumu hili la kutarjum kitabu hiki, kutoka lugha yake ya asili ya Kiarabu kwenda lugha ya Kiswahili. Halikadhalika tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.