Fadhila-za-watukufu-watano-katika-sahih-sita

Fadhila-za-watukufu-watano-katika-sahih-sita

Fadhila-za-watukufu-watano-katika-sahih-sita

Interpreter :

Hemedi Lubumba

Publication year :

2013

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Fadhila-za-watukufu-watano-katika-sahih-sita

Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha Kiarabu na kinaitwa, Fadha’ilu ‘l-Khamsah min Sihah Sittah, kilichoandikwa na mwanachuoni mahiri aitwaye Sayyid Murtadha al-Husaini al- Firuzabadi. Sisi tumekiita, Fadhila za Watukufu Watano katika Sahih Sita. Kitabu hiki ni matokeo ya utafiti uliofanywa na mwanachuoni huyu juu ya utukufu na fadhila za watukufu watano kutoka katika vitabu sita maarufu vya wanavyuoni mashuhuri wa Kisunni viitwavyo, Sihaa Sittah. Ni jambo la kupendeza kwamba pamoja na kuhitilafiana baina ya Sunni na Shia lakini kuna mambo mengi ya kimsingi ambayo wote wanakubaliana; na cha kufurahisha zaidi ni kwamba mambo hayo yamehifadhiwa vizuri katika vitabu vya historia na hadithi vya wanavyuoni wote Shia na Sunni. Mwandishi wa kitabu hiki amechagua kufanya utafiti wake kwenye vitabu vya Sahih Sita vya Sunni ambavyo ni vitabu vikubwa vya hadithi kwa upande wa ndugu zetu Masunni. Utafiti huu ni kwa ajili ya kuelimishana tu na si vinginevyo. Kusema kweli ni muhimu sana kujua imani za watu wengine kupitia vyanzo vyao wenyewe vilivyo sahihi badala ya kutafuta habiri hizo kupitia vyanzo ambavyo sio sahihi na wala si vya kuaminika, na matokeo yake kuleta malumbano yasiyo na natija katika jumuiya yetu ya Waislamu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Al-Haj Hemedi Lubumba Selemani kwa kazi kubwa aliyofanya ya kukitarjumi kwa Kiswahili; pia na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera. Amin