Familia ya Kiislamu

Familia ya Kiislamu

Familia ya Kiislamu

Publication year :

2004

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Familia ya Kiislamu

Juzuu hii imekusudiwa kuwawezesha wasomaji kufahamu vyema umuhimu wa ndoa, lengo lake katika Uislamu pamoja na wajibu wa mume na mke katika familia. Imekusudiwa kuwawezesha wanandoa, ikibidi, watalikiane kwa wema. Imekusudiwa vile vile iwaelekeze Waislamu namna ya kurithi au kurithishana Kiislamu. Aidha, juzuu hii huwaongoza wasomaji kubaini hila na upogo uliomo katika kampeni za kudhibiti uzazi.
Na zaidi inatarajiwa wasomaji waweze kuona zile haki, heshima na hadhi kubwa aliyonayo mwanamke katika Uislamu, ambazo hazipati mwanamke yeyote katika mifumo ya maisha ya kijahiliya.
Hivyo basi, baada ya wasomaji kuipitia juzuu hii kwa makini, inatarajiwa watakuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kuhuisha Uislamu katika jamii, wakitumia neema ya mali, nguvu, vipawa na muda aliowajaalia Allah(s.w), kama walivyofanya Mitume na watu wema waliotangulia.