Hadithi Qudsi
Hadithi Qudsi
Author :
Interpreter :
(0 Kura)
(0 Kura)
Hadithi Qudsi
Sifa zote njema anastahiki Allah (s.w.t.) aliyeumba ulimwengu na kusimamisha mbingu bila nguzo, kwa hakika yeye husikiliza dua zetu tuanazosoma na husikiliza hata tukimtaja kwa siri. Yeye ndiye anayetangua mateso, misiba, kuondosha kiza, kutakasa mioyo yetu. Kwa kupitia rehema, hujalia matumaini kwa wale waliokata tamaa. Yeye hudhihirisha ukarimu wake ambao hauna mfano na kuwajalia riziki binadamu kupita kiwango kinachohitajika. Salam ziwe kwa mitume yake yote aliyotutumia pamoja na maimamu wa haki aliowatakasa na khasa kwa mpenzi wake Muhammad Al-Mustafa (s.a.w.) ambaye ni lakiri wa mitume. Hakika ni neema kubwa mno ya Allah (s.w.t.) licha ya kutufundisha namna ya kumomba yeye lakini vile vile hata namna ya kuzungumza na yeye kupitia dua. Kupitia hizo dua mtu hugundua kuna ruwaza ya ukarimu na wema. Ikiwa binadamu atatengana na silisili (pattern) zilizo pandikizwa na waovu, basi kwa hakika binadamu amejaliwa uwezo kujiokoa nafsi yake kutokana na khofu inayomkabili katika maisha yake ya kila siku, hiyo itaweza kumgeuza binadamu kuwa kiumbe mtiifu na mwabudu wa Allah (s.w.t.) tu ambalo ndio lengo la kuumbwa kwake. Hizi Hadith Al-Qudsi ni tarjuma ya kitabu Al-hadith al-qudsi kilichotarjumiwa na ndugu N. M. Walji wa Nairobi chini ya uangalizi wa Seyyid Murtadha M. Murtadha.