Hatimaye-Nimeongoka

Hatimaye-Nimeongoka

Hatimaye-Nimeongoka

Publication year :

2002

Publish location :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Hatimaye-Nimeongoka

Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tarjuma ya Kitabu cha Kiarabu, kiitwacho Thummah-tadaytu, kilichoandikwa na Shaikh Muhammad Tijani Samawi wa Tunisia. Katika Kitabu hiki ameelezea kuhusu safari yake kuelekea kwenye Imani ya Kishi‘a. Kitabu hiki kimekuwa maarufu katika ulimwengu wa Kiislamu na tayari kimetafsiriwa katika lugha za Kiingereza, Urdu na Kiajemi. Wanachuoni wengi katika Afrika ya Mashariki wametuomba tukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili pia. Nilimuomba Shaikh Musabbah Sha’ban Mapinda kukitarjumi kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake ya lugha ya Kiarabu. Namshukuru kwa kukubali ombi langu na kuifanya kazi hii kwa moyo mkunjufu. Nimeiangalia pamoja naye tarjuma hii kwa makini kuhakikisha kuwa maudhui yake ya asili hayakupotoshwa katika lugha ya Kiswahili. Tunamshukuru Allah Subhanahu wa Ta‘ala na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine kwa kufanikisha kuchapishwa kitabu hiki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) awalipe malipo mema hapa Duniani na baadaye huko Akhera. Amin.