IKHLÂS NA TAQWÂ

IKHLÂS NA TAQWÂ

IKHLÂS NA TAQWÂ

Interpreter :

Shuaıbu Kıfea

Publication year :

2014

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

IKHLÂS NA TAQWÂ

Shukurani na Sifa zote njema Anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye ameumba umbile la ulimwengu na kumweka
mwanadamu kileleni mwa sanaa Yake hiyo, pia Akamfunulia wahyi kumpa Ujuzi, Ikhilaswi na Taqwa.
Swala na Salamu zimshukie Nabii Muhammad (s.a.w) ambaye ndiye njia ya ulimwengu, nuru ya upendo, mwangaza
wa uwongofu na nyota ya jaha, yeye ndiye kigezo kikuu cha Ikhilaswi na Taqwa. Maisha ya mwanadamu daima hutumika kwa namna moja au nyingine. Jambo muhimu ni jinsi gani yatumike, ama yatumike katika uchaMungu na yawe ya ikhilaswi Kwake au yatumike katika ujahili na yasiwe na maana yoyote.
Mambo muhimu zaidi yanayofanya maisha ya mtu yawe na maana ni taqwa (uchamungu) na usafi wa moyo(ikhilas).
Taqwa ni kule kuyadhibiti matamanio ya kimwili na kuimarisha nguvu ya kiroho kwa njia ya swala za kumuelekea Mwenyezi Mungu na kuwatendea wema binadamu. Hivyo basi, taqwa huhitajika katika kila eneo la maisha, katika imani zetu,ibada zetu, mahusiano yetu na wengine, na hata katika kila pumzi ya uhai wetu.
Kuwa na taqwa maana yake ni kuwa rafiki wa Mwenyezi Mungu, kuwa na moyo wenye siha ya imani hapa duniani,
moyo ambao unaweza kuzingatia mafunzo yatokanayo na ishara za uweza wa Mwenyezi Mungu ulimwenguni, na kuwa na buruhani ya kuingia Peponi kwa rehema za Mwenyezi Mungu.