ili_niwe_pamoja_na_wakweli

ili_niwe_pamoja_na_wakweli

ili_niwe_pamoja_na_wakweli

Publication year :

2001

Publish location :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

ili_niwe_pamoja_na_wakweli

Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho Liakuuna Ma'as-Sadiqin kilichoandikwa na Shaikh Muhammad Tijani Samawi wa Tunisia. Ndani ya Kitabu hiki ameelezea mkusanyiko wa itikadi za Kiislamu kwa namna zilivyo ndani ya Qur'an na Sunna Tukufu ya Mtume (s.a.w.w.). Kitabu hiki ni kama kile cha mwanzo, nacho kimepata umaarufu hasa kutokana na jinsi mwandishi alivyozichambua itikadi hizo kwa mujibu wa mtazamo wa Sunni na Shia, kisha akayabainisha maeneo wanayohitilafiana. Kwa mara nyingine tena mimi binafsi sikusita kumuomba Shaikh Musabah Shaban Mapinda kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake ya lugha ya Kiarabu. Sababu iliyoifanya Mission yetu isimamie kazi hii ni kama ile ya kwanza, ambayo inatokana na maombi ya Maulamaa wengi katika Afrika Mashariki kututaka tukifasiri kitabu hiki kiingie kwenye lugha ya Kiswahili. Namshukuru Shaikh Musabah kwa kukubali ombi langu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja. Nimeiangalia pamoja naye tafsiri hii kwa makini kuhakikisha kuwa maudhui yake ya asili hayakupotoshwa katika lugha ya Kiswahili. Shaikh Tijani Samawi ameandika vitabu zaidi ya hivi, na. Sheikh wetu Musabah Shaban Mapinda ametafsiri kitabu kingine cha mwandishi huyu kiitwacho Fa'salu Ahlad-Dhikri (Waulizeni wanaofahamu) ambacho tayari kimeshapangwa katika kompyuta. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tena kwani kitabu chetu cha "Hatimaye Nimeongoka" kimependwa mno na wasomaji na hivyo kutupa ari ya kuchapisha hiki ulichonacho mkononi na kitakachofuatia Insha-Allah. Ushahidi wa kupendwa kwa kitabu hicho ni shukurani na pongezi tunazozipokea toka kwa wasomaji kwa namna mbalimbali ikiwemo kutuandikia barua n.k. Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa mfasiri na kwa wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine katika uchapishaji wa kitabu hiki.