Imam Ali Ndugu yake Mtume Muhammad (sehemu ya kwanza ya juzuu ya kwanza)
Imam Ali Ndugu yake Mtume Muhammad (sehemu ya kwanza ya juzuu ya kwanza)
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2012
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Imam Ali Ndugu yake Mtume Muhammad (sehemu ya kwanza ya juzuu ya kwanza)
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, The Brother of the Prophet. Sisi tumekiita, Imam Ali (as) Ndugu wa Mtume Muhammad (saw). Kitabu hiki kilitungwa na aliyekuwa muballighi mashuhuri wa dini ya Kiislamu ya Ushia nchini Marekani, Marehemu Sheikh Muhammad Jawad Chirri. Kitabu hiki ni wasifu wa mtu mkubwa ambaye alikuwa mwanamume wa kwanza kuamini Utume wa Muhammad (saw) na wa kwanza kusali nyuma yake. Imam Ali (as) hakuwa kiongozi wa Waislamu tu bali wa wanadamu wote. Maisha na mwenendo wa Imam Ali (as) umewavutia watu wote, marafiki na maadui, hali ambayo imemfanya kuwa kiongozi wa umma. Mtukufu Mtume (saw) alimtangaza mwanzoni kabisa mwa Ujumbe wake katika kile kikao mashuhuri kabisa cha “karamu ya jamaa”, aliposema: “Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu, waziri wangu, khalifa wangu na mrithi wangu. Basi msikilizeni na mumtii.” Hili lilikuwa tangazo la mwanzo kabisa alilolitoa Mtukufu Mtume (saw) kwa ajili ya Imam Ali (as) na aliendelea kuwakumbusha Waislamu kuhusu uongozi wa Imam Ali baada yake katika matukio mengi yaliyofuata baadaye, kama vile katika tukio la Ghadir Khum pale aliposema: Man kuntu mauwahu fahadha Aliyyun mawlahu – Yule ambaye mimi kwake ni kiongozi basi na huyu Ali ni kiogozi wake.” Na mwisho ni tukio la “Karatasi” pale Mtukufu Mtume (saw) alipokuwa ni mgonjwa na maradhi yamemzidi akaomba aletewe karatasi, kalamu na wino, mashuhuri kama “Hadithi ya karatasi.” Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.