IMAM HUSEIN (A.S.) NI UTU NA KADHIA
IMAM HUSEIN (A.S.) NI UTU NA KADHIA
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2014
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
IMAM HUSEIN (A.S.) NI UTU NA KADHIA
Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha yaKiarabu kwa jina la, al-Imam Husayn ash-Shakhsiyyatun wa 'l-Qad-hiyyah, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisitumekiita, Imam Husain (a.s.) ni Utu na Kadhia.Imam Husain (a.s.), mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)alikataa kula kiapo cha utii kwa mtawala dhalimu na badala yakeakaamua kujitoa muhanga kwa ajili ya kuinusuru dini ya Allah ku-tokana na upotoshaji uliokuwa ukifanywa na mtawala dhalimu wawakati huo - Yazid bin Muawiya bin Abu Sufyan.Imam Husain aliishi kwa malengo makubwa ya kuwasaidia nakuwakomboa wanyonge kutokana na ukandamizaji wa watawalamadhalimu, na hususan kuurudishia Uislamu heshima yake.Kwa hakika hakuinusuru tu dini ya Allah, bali pia alijitoa muhangakwa ajili ya wanyonge na wanaokandamizwa ulimwenguni pote. Hiindio maana kila mwaka inapofika mwezi wa Muharram, Waislamuulimwenguni kote hukusanyika si kwa ajili ya kuomboleza tu, balipia kukumbushana yale ambayo Imam (a.s.) aliyatolea muhanga nakuhimizana kuyasimamia na kuyafanyia kazi.Mwandishi wa kitabu hiki anatumia kalamu yake kuelezea harakatiza Imam Husain (a.s.) zilivyoinusuru dini ya Allah na kuwakomboawanyonge na wanaokandamizwa ulimwenguni pote. Azma yake nikuendeleza harakati hizo katika ulimwengu huu wa sasa ambaoakina Yazid bado wapo na wanaendelea kujitokeza kila wakati.Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususanwakati huu ambapo watawala mabeberu na madhalimu wamezidishambio zao za kuwakandamiza wanyonge na kuyakandamiza nakuyaonea mataifa madogo ulimwenguni kwa kuanzisha vita bainayao na kupora rasilimail zao.Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua ku-kichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yakeyaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji waKiswahili.Tunamshukuru ndugu yetu Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kazikubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutokalugha ya asili ya Kiarabu. Aidha tunawashukuru wale wotewalioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikishakuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa dunianina kesho Akhera – Amin.