IMAM MAHDI NA BISHARA YA MATUMAINI

IMAM MAHDI NA BISHARA YA MATUMAINI

IMAM MAHDI NA BISHARA YA MATUMAINI

Publication year :

2014

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

IMAM MAHDI NA BISHARA YA MATUMAINI

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni kitabu asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, al-Imam Mahdi wa Basha'ira 'l-Amal, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa al-Saffar. Na sisi tumekiita, Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini. Imam Mahdi (a.s.) ni Imam wa kumi na mbili na wa mwisho kati ya Maimamu watokanao na Ahlul Bayt (a.s.) na ambao hufuatwa na wafuasi wa madhehebu ya Shia Ithna Asharia. Imam Mahdi (a.s.) yuko hai na katika Ughaibu (kutoonekana) na atadhihiri tena Allah atakapopenda na wakati huo ulimwengu utakuwa umejaa dhulma na yeye ataujaza kwa haki na uadilifu. Huyu ndiye Imam wa zama hizi na ni muhimu kila Mwislamu kumtambua, kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amenukuliwa akisema kwamba mtu asiyemtambua Imam wake wa zama na akafa katika hali hiyo atakuwa amekufa kifo cha kijahilia (yaani cha kikafiri). Mwandishi wa kitabu hiki anatumia kalamu yake kuelezea kwa ufupi wasifu wa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) na umuhimu wake katika zama hizi. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo watawala mabeberu na madhalimu wamezidisha mbio zao za kuwakandamiza wanyonge na kuyakandamiza na kuyaonea mataifa madogo ulimwenguni kwa kuanzisha vita baina yao na kupora rasilimail zao. Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Aidha tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin.