Drawer trigger

Ismah ya Mitume katika Qur’an

Ismah ya Mitume katika Qur’an

Ismah ya Mitume katika Qur’an

Mwaka wa uchapishaji :

2008

Eneo la uchapishaji :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Ismah ya Mitume katika Qur’an

Kitabu kilochopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha kiingreza kiitwacho The Infallibility of the Prophets kilichoandikwa na mwanachuoni maarufu Hujjatul Islam Wal Muslimeen Al-Haj Sayyid Muhammad Rizvi wa Toronto, Canada. Sababu iliyoifanya Bilal Muslim Mission isimamie kazi hii ni kama zile za mwanzo, ambazo zinatokana na maombi ya watu wengi kutoka Afrika ya Mashriki kututaka tuifasiri kitabu hiki muhimu katika lugha ya Kiswahili pia. Mimi binafsi sikusita kumuomba ndugu yetu Al-Haj Dr. Muhammad Salehe Kanju, Mwenyekiti wa Shia Centre, Bilal Muslim Mission Mkumbara, kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake ya Kiingereza. Namshukuru Dr. Kanju kwa kukubali ombi langu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja. Pia ninatoa shukrani kwa Asha Mohamed Mtulia na Shinuna Maulid Kambi kwa kukichapisha kwenye kompyuta na kukipanga. Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote ambao kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine katika kazi zetu za Tabligh ya Watukufu Ahlul~Bayt (a.s.). Tunamuomba Allah (s.w.t.) awalipe malipo mema hapo Duniani na baadaye huko, Akhera - Amin.