KHAIR ULBARIYYAH
KHAIR ULBARIYYAH
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2011
Publish location :
Tanzania Dar es salaam
(0 Kura)
(0 Kura)
KHAIR ULBARIYYAH
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Khayru ‘l-Bariyyah ambacho sisi tumekiita kwa jina hilohilo. Jina la kitabu hiki linatokana na hadithi ya Mtukufu Mtume SAW kama ilivyosimuliwa na Ibn ‘Asakir kutoka kwa Jabir bin Abdallah kwamba alisema: “Tulikuwa pamoja na Mtume SAW wakati Ali AS alipokuja (hapo tulipokuwa tumekaa). Mtume akasema: ‘Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake; hakika huyu (Ali) na Shia (wafuasi) wake ndio wenye kufuzu Siku ya Ufufuo.’ Kisha aya ifuatayo ikashushwa: ‘Hakika wale walioamini na kutenda mema,basi hao ndio wema wa viumbe!’”1 Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu.