kumswalia-Mtume

kumswalia-Mtume

kumswalia-Mtume

Interpreter :

HARUN PINGILI

Publication year :

2011

Publish location :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

kumswalia-Mtume

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, as-Swalaatu ‘Ala ‘n-Nabii, kilichoandikwa na Sheikh Abdul Karim al-Bahahani. Sisi tumekiita, Kumswalia Mtume.Kitabu hiki kinazungumzia juu ya hitilafu zilizotokea juu ya maneno yanayosomwa katika kumswalia Mtume Muhammad SAW (Swallallaahu ‘Alayhi Wa-aalih). Baadhi ya wanavyuoni wanasema kwamba kumswalia Mtume ni kusema: “Allaahumma swalli ‘alaa Muhammad” bila kuongeza kitu. Wengine wanasema kumswalia Mtume ni kusema: “Allaahumma swalli ‘alaa Muhammad wa Aali Muhammad” kama utakaavyoona maelezo yake ndani ya kitabu hiki. Sheikh wetu huyu amefanya utafiti wa kina juu ya suala hili na kuonyesha kwa uwazi na pasina shaka yoyote juu ya asili ya swala ya Mtukufu Mtume. Mwanachuoni huyu mtafiti ametumia vyanzo halisi na sahihi katika kulifikia lengo lake hili. Vyanzo hivyo si vingine bali ni Qur’ani na Sunna, pamoja na matukio ya kweli ya kihistoria, akili, mantiki na elimu. Kutokana na umuhimu wa maudhui hii tumeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kutoa mwanga kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili juu ya suala hili ambalo linawatatiza na kujua ukweli wake. Tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Haroon Pingili kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote ambao wameshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.