KWA NINI MASHIA HUSUJUDU JUU YA UDONGO?
KWA NINI MASHIA HUSUJUDU JUU YA UDONGO?
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
1990
Number of volumes :
2500
Publish number :
Toleo ya Pili
Publish location :
Dar es Salaam, Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
KWA NINI MASHIA HUSUJUDU JUU YA UDONGO?
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa shukrani nyingi kwa kunipa uwezo wa kuendeleza matamanio yangu ya kufasiri na kuandika vitabu vya kidini kwa lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha ndugu zetu wa Kiafrika kupata maarifa zaidi ya dini ya ya Kiislamu kwa kupitia Madhehebu ya Ahlul-Bait wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) ijulikanayo kwa Jina la “Shia Ithna-ashari.” Baada ya kutunga kitabu “Mambo Yanayomhusu Maiti”, nimeona ni afadhali na fardhi kwangu kujishughulisha na masuala yanayowakera Waislamu wengi wasiojua miongoni mwa ndugu zetu wa Kisunni; ambayo bila sababu ya maana na msingi wowote huleta tuhuma, chuki na utengano kati ya Waislamu. Moja katika masuala hayo yanayoulizwa na ndugu zetu ni, “Kwa nini Mashia husujudu juu ya udongo?” Kusita kwao kutafiti jibu lake katika vitabu vyao wenyewe kunawafanya watutuhumu sisi eti kwamba tunavisujudia na kuviabudu vipande vya udongo!!! Kijitabu hiki ni tafsiri ya sehemu moja ya kitabu kiitwacho سیرتناوسنتنانبینا (صلی الله علیه وآل وسلم)وسنته (Mienendo Yetu na Sunna Zetu ni Mienendo ya Mtume Wetu (s.a.w.w) na Sunna Zake) kilichoandikwa na mwanachuoni mashuhuri wa Kishia, Hayati Allamah Sheikh Abdul-Hussain Al-Amini. Mtungaji huyu ameandika vitabu vingi vyenye kutoa majibu ya masuala yanayowatatiza ndugu zetu wa Kisunni. Kimoja katika vitabu vyake vilivyo maarufu ni kile kinachoitwa Al-Ghadir. Katika kitabu hiki, Allamah Al-Amini hakuacha kunukuu japo hadithi moja kutoka katika vitabu maarufu vya wanavyuoni mashuhuri wa Kisunni yenye kuthibitisha jambo hili. Mtungaji amezigawa hadithi hizo katika mafungu matatu. Sehemu ya kwanza ni zile Hadithi zenye kuonyesha kwamba ni lazima kusujudu katika ardhi unaposujudu katika sala. Suhumu ya pili ni ni zile Hadithi zinazoruhusu kusujudu juu ya vitu vingine badala ya ardhi (kwa mfano mkeka) bila ya udhuru wowote na Sehemu ya tatu ni zile Hadithi zinazomruhusu mwenye udhuru kusujudu juu ya vitu vingine badala ya ardhi. Mwishowe, Allama Amini amethibitisha ubora na umuhimu wa kusujudu juu ya udongo mkatifu wa Karbala kwa sababu ya kuhusika na Mwenyezi Mungu. Tunamwomba Mwenyezi Mungu kwa baraka ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bait (a.s.) wake atupe Taufiki ya kutuwezesha kuendelea kuwaelezea ndugu zetu sunna halisi za Mtukufu Mtume (s.a.w.).