Kwa Nini Uislamu Umemruhusu Mume Kuoa Wake Wengi
Kwa Nini Uislamu Umemruhusu Mume Kuoa Wake Wengi
Author :
Publisher :
Publication year :
1984
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Kwa Nini Uislamu Umemruhusu Mume Kuoa Wake Wengi
Ndoa ya Wake wengi: Jambo hili laonekana lenye kuchukiza kiasi gani! Jambo la kushangaza hasa ni kuwa wale watu wanaojaribu kushawishi fikara za muundo wa jamii ambazo huzifikiria ndoa za wake wengi kuwa ni jambo
liruhusiwalo tu lakini si la lazima, na ambao hufikiria kuwa muundo wa mume mmoja kwa mke mmoja ndio muundo thabiti na ufaao kwa ustaarabu, wanaziona ndoa za wake wensi kuwa ni jambo lenye kuchukiza sana.
Watu hawa wanaelewa wazi kuwa haiwezekani kuweka sheria ambayo inamtosheleza mwanaume kwa mke mmoja tu. Watu hawa hawa wanaoyahubiri mapenzi ya mume mmoja kwa mke mmoja, wanaonekana kuwa wameanza kufanya mapenzi haramu au mambo fulani fulani na watu wengine.
Watu hawa wamuonapo Mwislamu mwaminifu mwenye wake wawili wapatao mapenzi ya sawa sawa kutoka kwa mume wao, na ambaye hafanyi mapenzi haramu maishani mwake, huanza kumdharau na kuichukia ndoa ya
wake wengi, huku wakitoa mifano kujaribu kuonyesha kuwa maisha ya namna hiyo ni jambo lisilowezekana.
Si kweli kuwa mtu karuhusiwa kuwa na wake wengi kwa ajiii ya kujitosheleza kiashki tu, Shabaha ya kuruhusiwa kwa ndoa za wake wengi ni kujaribu kukomesha tabia mbaya katika jamii na kuzuia fujo. Tendo la mume kuoa wake
wengi humfanya mke na mume wajitosheleze, na wakati huo huo kuisalimisha jamii kutokana na kutawanya wapenzi kila mahali katika jamii hiyo. Jamii ya namna hii inaweza kujengwa tu kwa kuwaruhusu watu kuoa wake wengi.
Kwa vile ndoa ya wake wengi ni jambo lenye kuleta mabishano, jambo hili linahitaji kufikiriwa sana na kuhojiana. Tukiachilia mbali kule kudumisha ndoa halali kati ya mume mmoja na wake wengi, hebu natulitazame wazo hili, kwa kuzitazama lawama za watu wa nchi za Magharibi na kuona ni wapiwalipokosea. Kitabu hiki kinatoa hoja zenye kuunga mkono ndoa ya wake wengi katika njia ya waziwazi kabisa.