Maisha-binafsi-ya-Ahlulbayt-as

Maisha-binafsi-ya-Ahlulbayt-as

Maisha-binafsi-ya-Ahlulbayt-as

Interpreter :

Amiri Mussa Kea

Publication year :

2017

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Maisha-binafsi-ya-Ahlulbayt-as

K itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, al-Hayatu ‘sh-Shakhsiyyah ‘inda Ahlu‘l-Bayt kilichoandikwa na Sheikh Fawzi Aali Saif. Sisi tumekiita, Maisha Binafsi ya Ahlul Bayt (a.s.).
Maisha ni kupanga, na kupanga ni kuchagua. Kuchagua maana yake kuchukua kilicho bora na kuacha kilicho kibaya, na katika maisha maana yake ni kuishi maisha mazuri na yenye maadili mema na kuamiliana vizuri na binadamu wenzako kwa ubinadamu wenu bila kujali itikadi zenu, kabila au rangi, na kuamiliana vizuri na waumini wenzako kama ndugu zako katika imani. Ili kuyafikia malengo haya, huna budi kupata malezi bora ya kiroho na kimwili kuanzia utotoni. Wazazi ndio chimbuko la kwanza la malezi haya, lakini kuna kufunzwa na wazazi na kufunzwa na
ulimwengu. Mambo haya hayawezekani mpaka apatikane mwalimu mzuri wa kufundisha somo hili.
Allah Mwingi wa rehema kwa huruma Zake na Upole kwa viumbe Wake akawa anawatuma Wajumbe miongoni mwa viumbe Wake mara kwa mara kuanzia alipomuumba mwanadamu ili kuwafundisha maadili mema pamoja na kumjua Yeye kama Muumba wao. Kuwatoa katika hali mbaya na kuwapeleka katika hali nzuri,kuwatoa katika giza na kuwapeleka kwenye mwanga. Allah ‘Azza wa Jallah ametuma takriban Wajumbe (Mitume) 124,000 wa kwan-
za akiwa ni Nabii Adam (a.s.) na wa Mwisho ni Nabii Muhammad (s.a.w.w.) ambaye amemtaja kwamba kuwa ni rehema kwa walimwengu wote. Hii ina maana kwamba si kwa wanadamu tu bali hata kwa viumbe wengine kama wanyama, n.k. Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ametajwa katika Qur’ani Tukufu kuwa ni “kiigizo chema” (uswatun hasanah). Mwenendo wake wote wa maisha ni somo kwa wanadamu wote. Na alipofariki akatuachia vitu viwili Qur’ani Tukufu iliyosheheni mfumo wote wa maisha kwa mwanadamu, na watu wa nyumbani kwake Ahlul Bayt (a.s.). Akutuusia kwamba ili tufanikiwe katika maisha yetu ya hapa duniani na Akhera, basi tushikamane na vitu hivyo vizito viwili (yaani Qur’ani na Ahlul Bayt wake watoharifu).Mwandishi katika kitabu hiki anaonesha jinsi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul Bayt wake ambao ni Maasumina 12 (a.s.) walivy oishi ili tuige mfano wao na ili tuishi maisha bora na maadili mema.
Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao. Tunawashukuru ndugu yetu al-Haj Ustadh Amir Musa Kea kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Amin!