Majlisi-za-Imam-Hussein-majumbani
Majlisi-za-Imam-Hussein-majumbani
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2011
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Majlisi-za-Imam-Hussein-majumbani
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu kiitwacho , al-Majaalis al-Husayniyyah Fi ‘l-Buyuut kilichoandikwa na Jamil Kamal. Sisi tumekiita, Majlisi za Imam Husain AS Majumbani.
Kila mwaka mwezi wa Muharram, Waislamu hususan Mashia, hukusanyika katika kumbi maarufu ziitwazo Husainia , Mahfil au Imambara, n.k. kuomboleza kuuawa shahidi Imam Husain AS, mjukuu wa Mtukufu Mtume SAW, katika ardhi ya Karbala (Iraq). Katika kitabu hiki mwandishi anashauri zifanyike majlisi ndogondogo majumbani zisizo na gharama kubwa na ambazo kwa uzoefu wake ameziona kuwa zina matokeo mazuri sana.
Sisi tumeuona ushauri huu kuwa ni mzuri sana, na kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili wasomaji wetu, hususan Waislamu, wazungumzaji
wa Kiswahili waufanyie kazi ushauri huu.
Tunamshukuru Abdul Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa na changamoto kubwa kwa wasomaji wetu.