Mashairi ya kijamii
Mashairi ya kijamii
Author :
Editor :
Publisher :
Publication year :
2015
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Mashairi ya kijamii
M ashairi ni sanaa muhimu sana katika jamii, katika kufikisha ujumbe wa aina mbalimbali, katika kuipa jamii taarifa zinazojiri ndani ya jamii yao, na katika jumuiya zao na ulimwenguni kwa ujumla. Ni kwa kupitia sanaa hii jamii huhamasishwa kushiriki katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo yao na ya nchi yao. Halikadhalika sanaa hii ni burudani maridhawa katika jamii inayohusika. Katika kitabu hiki tunawaletea wasomaji wetu mashairi yaliyotungwa na malenga wetu, Ndugu Juma S. N. Mgambilwa.
Katika kitabu hiki mshairi ameandika kuhusu kadhia mbalimbali zilizotokea hapa nchini, k.v. ustawi wa jamii, vijana, uongozi, uadilifu wa viongozi, tabia njema n.k. Ameshughulikia jumla ya mada 50.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa, husasan wakati huu ambapo jamii nyingi ikiwemo ya kwetu zinashuhudia uporomokaji mkubwa wa maadili Tunamshukuru ndugu yetu mtunzi wa mashari haya kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuandika na kuyakusanya mashairi haya katika kitabu hiki mlichonacho mikononi mwetu. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera pia. Amin!