Maswali na Majibu

Maswali na Majibu

Maswali na Majibu

Interpreter :

Amiri Mussa Kea

Publication year :

2011

Publish location :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Maswali na Majibu

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiajemi kiitwacho, Pasokh be Barkhi Shubahat-e Madhhabi (Majibu ya Baadhi ya Maswali Yenye Utata). Sisi tumekiita, Maswali na Majibu. Kitabu hiki kiko katika mtindo wa maswali na majibu. Haya ni maswali ambayo Waislamu wengi, hususan wale ambao sio wa madhehebu ya Shia, imma wanauliza au huwahusisha Mashia na baadhi ya matendo ambayo wao huyaona kuwa ni uzushi (bidaa) na kuwashutumu nayo. Mwandishi wa kitabu hiki amekusanya baadhi ya maswali na shutuma hizo wanazotupiwa Mashia na kuyapanga maswali na shutuma hizo katika kitabu hiki kwa mpango wa maswali na majibu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahilikwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.