Misingi-ya-Itikadi-kwa-vijana

Misingi-ya-Itikadi-kwa-vijana

Misingi-ya-Itikadi-kwa-vijana

Publication year :

2017

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Misingi-ya-Itikadi-kwa-vijana

K itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, Usulu ‘l-‘Aqaid li ‘sh-Shabab kilichoandikwa na Sheikh Nasir Makarim Shirazi. Sisi tumekiita, Misingi ya Itikadi kwa Vijana.
Mwandishi katika kitabu hiki ameshughulikia kwa upeo zaidi suala la itikadi ambalo kwalo baadhi ya wanazuoni na madhehebu za Kiislamu wamehitilafiana. Kwa mfano, suala kuonekana kwa Mungu hapa duniani na Akhera. Wako wanaosema ataonekana Akhera kwa waumini tu, wengine wanasema ataonekana hapa duniani na Akhera pia, lakini wengine wanasema kwa uhakika kabisa kwamba kamwe hataonekana si hapa duniani wala Akhera. Sasa ili kuyaelewa yote hayo fuatana na mwandishi wa kitabu hiki.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa hususan wakati huu wa sayansi na tekinolojia kubwa ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi kwa watu wa sasa.
Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao.
Tunamshukuru ndugu yetu Ustadh Abdul Karim Juma Nkusui kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Amin!