MIUJIZA KATIKA MIILI YETU

MIUJIZA KATIKA MIILI YETU

MIUJIZA KATIKA MIILI YETU

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

MIUJIZA KATIKA MIILI YETU

Katika vitabu vyote vya mwandishi huyu, masuala yanayohusu imani yamefafanuliwa kwa muongozo wa Aya za Qur’an na watu wanapewa wito kujifunza maneno ya Mwenyezi Mungu na kuishi kwa mujibu wake. Mada zote zinazohusu Aya za Mwenyezi Mungu zimefafanuliwa katika namna ambayo haiachi shaka au alama za viulizo katika akili ya msomaji. Mtindo wa ukweli, uwazi na ufasaha uliotumika unamhakikishia kila mtu wa rika lolote na wa kundi lolote la kijamii kuwa anaweza kuvielewa vitabu hivi kwa urahisi. Simulizi hii halisi na yenye kueleweka kwa urahisi itakuwezesha kuvisoma kwa mkupuo mmoja. Hata wale wanaokana vikali mambo ya kiroho huvutiwa na mambo ya hakika yaliyoelezwa katika vitabu hivi na hawawezi kuyakana maelezo yake yenye ukweli. Kitabu hiki na vitabu vyote vya mwandishi huyu vinaweza kusomwa na mtu mmojammoja au katika vikundi wakati wa mazungumzo. Wasomaji wanaotaka kufaidika na vitabu hivi watakuta kuwa mfumo wa majadiliano unafaa sana kwa maana kwamba wataweza kuwaeleza wenzao juu ya hisia na uzoefu wao. Aidha, itakuwa ni mchango mkubwa kwa dini kugawa vitabu hivi wakati wa kuwasilisha na usomaji wa vitabu hivi ambavyo vimeandikwa kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu pekee. Vitabu vyote vya mwandishi ni vyenye ushawishi na mvuto mkubwa. Kwa sababu hii, mojawapo ya mbinu zenye athari kubwa kwa wale wanaowahubiria dini watu wengine ni kuwahamasisha vitabu hivi.