MKUSANYIKO WA SIFA NA TAREHE ZA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.), IMAMU ALI, BIBI FATIMAH, IMAMU HASSAN NA IMAMU HUSSEIN

MKUSANYIKO WA SIFA NA TAREHE  ZA  MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.), IMAMU ALI,  BIBI FATIMAH, IMAMU HASSAN NA  IMAMU HUSSEIN

MKUSANYIKO WA SIFA NA TAREHE ZA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.), IMAMU ALI, BIBI FATIMAH, IMAMU HASSAN NA IMAMU HUSSEIN

Interpreter :

HARUN PINGILI

Publication year :

2003

Publish number :

Chapa ya Tatu

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

MKUSANYIKO WA SIFA NA TAREHE ZA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.), IMAMU ALI, BIBI FATIMAH, IMAMU HASSAN NA IMAMU HUSSEIN

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Kila sifa njema na shukrani ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa Ulimwengu. Rehema na amani zimshukie Mtume Muhammad, Jamaa (Aali) zake, na Sahaba zake. Marhum Sheikh Abdullah Saleh Farsy amefanya kazi kubwa juu ya Uislamu kwa kutunga MAISHA YA NABII MUHAMMAD (s.a.w.w. - Sallallahu Alaihi wa Aalihi wa sallam). Ni muhimu sana kwa kila Mwislamu kukijua kitabu hiki, kwa sababu kimekusanya tarehe na sifa za Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Kadhalika, Marhum Sheikh Muhammad Kasim Mazrui amefuatisha vitabu juu ya Makhalifa wanne, baada ya Mtume (s.a.w.w.), navyo ni: 1) Maisha ya Abubakar Asiddik, 2) Maisha ya Umar Al-Faruk, 3) Maisha ya Uthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. Vitabu hivi vinne ni muhimu sana na nafuu kubwa kwa Waislamu wa Afrika Mashariki, kwa sababu vinaeleza kwa Kiswahili tarehe ya Uislamu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Ninawahimiza sana Waislamu, wakubwa na watoto, wavisome vitabu hivyo vitano. Mungu awalipe malipo mazuri Marhum Sheikh Abdullah Saleh Farsy na Marhum Sheikh Muahammad Kasim Mazrui, na vizazi vyao, Ninamwomba duniani na Akhera - Amen. Mimi nimeona vizuri nifuatishe vitabu hivyo kwa kutunga kitabu juu ya tarehe ya AHLUL-BAYT (Watu wa Nyumbani mwa Mtume (s.a.w.w.)) na nikakipa jina la AHLUL-KISAA (Watu wa Kishamia). Sikutaja tarehe ya watoto wote wa Mtume, wala tarehe ya Wake zake, (Radhiallahu Anhum Ajmaeen - R.A.A.) lakini nimetaja tarehe za wale tu walioingizwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) mwenye KISAA, nao ni Fatimah, Ali, Hassan na Hussein (Alaihimus Salaam - A.S). Makusudio yangu ni kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, ambaye alimwambia Mtume wake awaambie Waislamu: “.... Sema (ewe Rasuli Wetu Muhammad); Kwa haya (huku kukubalighishieni Ujumbe wa Allah) sikuombeni ujira wowote, ila mapenzi (yenu) kwa jamaa (zangu)........” (Ash-Shuura, 42:23) Namwomba kila atakayeona makosa katika kitabu hiki, asahihishe na anipe habari, kwani asiyekosa ni Mwenyezi Mungu tu.