MTUME WA REHMA MUHAMMAD

MTUME WA REHMA MUHAMMAD

MTUME WA REHMA MUHAMMAD

Interpreter :

Ibrahimu H. Kabuga

Publisher :

Erkam Printhouse

Publication year :

2022

Publish location :

Istanbul, Turkey

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

MTUME WA REHMA MUHAMMAD

Nilipoambiwa nitafsiri kitabu hiki kutoka katika lugha ya Kiingereza kwenda katika lugha ya Kiswahili, nilisita. Lakini, baada ya kukisoma kwa umakini, nilihamasika na kushawishika kuwa Waislamu na Wasiokuwa Waislamu
wanaozungumza Kiswahili watafurahia na watanufaika kwa
kujifunza kipengele muhimu cha maisha ya Mtume (s.a.w) ambacho kwa kawaida kimekuwa kikipuuzwa - kwa kukusudia au kwa kutokusudia. Kipengele kinachoelezwa na kukusudiwa katika kitabu hiki ni huruma ya Mtume (s.a.w), ambayo bila shaka, ndiyo nara (kauli mbiu) mashuhuri na maarufu ya maisha yake yote. Leo hii, Waislamu na wasiokuwa Waislamu wanahitaji kujua kuwa katika historia yote hakuna mtu yeyote anayeweza kuwa na huruma iliyojidhihirisha katika maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w). Wanatakiwa wajue kuwa mfano wake ni muhimu sana, hasa katika ulimwengu uliotawaliwa zaidi na choyo, ubinafsi na mitindo ya maisha ya kimaada. Kitabu hiki ni wito wa kuielekea Rehma katika uhusiano wetu wa kijamii na pia maingiliano yetu na mazingira kwa kuyatathmini upya maisha ya mfano ya rehma hii iliyoletwa kwa wanadamu wote, Mtume Muhammad (s.a.w) .