MUANDAMO WA MWEZI

MUANDAMO WA MWEZI

MUANDAMO WA MWEZI

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

MUANDAMO WA MWEZI

Baada ya hayo, sina budi kutoa shukurani na pongezi zangu za dhati kwa juhudi kubwa iliofanywa na ndugu zetu wa "Ansaru Sunna" Zanzibar kwa kutunga kitabu chao kujibu kitabu changu kuhusu miandamo ya mwezi. Mnamo mwezi Rajab, nilitumiwa meseji na mmoja wa ndugu zetu wa Zanzibar akiniambia "Je unajua kuwa kitabu chako cha mwezi kimejibiwa?" Nikamwambia sijui kwani sijaletewa kopi. Mara juzi tarehe 2/8/2009, nikajuilishwa na mmoja wa ndugu hapa Oman kuwa kitabu kimetumwa as soft copy katika E-Mail box yake. Kwa hivyo, nikafanya bidii ya kukipata ili nipate faida ya kile nisichokijua. Kwa bahati nilipokisoma sikuona kitu chochote cha kielimu, wala sikuona kwamba wameweza kuthibitisha dai lao kwamba muandamo mmoja ni hoja kwa walimwengu wote. Bali
kilichokuwemo ni "Juma kafanya hivi; Juma kasema hivi". Kwa kweli, kwa habari nilioletewa kotoka Zanzibar ni kuwa waliowengi wanasema kuwa hawakuweza kujibu hoja za kitabu chetu UshahdiUuliowekwa Wazi. Lakini
nami nasema kwamba wamejitahidi kadiri ya uwezo wao: kila ndege huruka kwa ubawawe.