Muujiza katika chembe ya Atomu
Muujiza katika chembe ya Atomu
Author :
Interpreter :
(0 Kura)
(0 Kura)
Muujiza katika chembe ya Atomu
Pamoja na wanasayansi kufanya jitihada kubwa za kitafiti kubaini ukubwa wake, mapana na umbali wake, ukubwa wa umbile la mbingu umepindukia uelewa wa Mwanaadamu licha ya kipawa kikubwa alichonacho cha akili yenye uwezo wa kutambua kila kitu. Mbingu hii na vilivyomo ndani yake vimetoka wapi? Vinaelekea wapi? Mwisho wake wapi? Na jinsi gani inavyofuata mtandao maalumu na wa pekee wa kutii sheria za kisayansi ambazo hazijulikani zilivyoanza? Kwa wanasayansi wazuri wanaotumia vipimo na mahesabu yenye uhakika ya maumbile ya mbingu na sayari zake, ni rahisi kwao kuliweka bayana suala hili kwa watu wenye kufikiri na kutafakari vizuri. Katika Qur’an tunaambiwa: Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuwatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonesha kuwapo Mwenyezi Mungu mmoja) kwa wenye akili. [Imran: 190). Kwa wanasayansi wanaoukana ukweli wa kuumbwa kwa mbingu na yaliyo baina yake wanapata taabu sana kujibu maswali magumu yanayojitokeza baada ya tafiti na ugunduzi mwingi wa kisayansi.