Mwenyezi Mungu na Sifa Zake

Mwenyezi Mungu na Sifa Zake

Mwenyezi Mungu na Sifa Zake

Interpreter :

Salman Shou

Publish location :

Dar es salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Mwenyezi Mungu na Sifa Zake

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la: "God and His Attributes." Sisi tumekiita: "Mwenyezi Mungu na Sifa Zake." Kitabu hiki, "Mwenyezi Mungu na Sifa Zake" ni kazi ya kielimu iliyofanywa na Mwanachuoni mahiri, Sayyid Mujtaba Musawi Lari. Mwandishi wa kitabu hiki ameichambua itikadi ya Kiislamu na Umoja wa Mungu (tawhid) kwa kutumia uhojaji wa kifilosofia na maneno mepesi. Ili kukamilisha kazi yake hii ametegemea sana juu ya Sunna na nukuu nyingi kutoka kwenye Qur'an Tukufu. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Salman Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.