NJIA YA ELIMU NA USTAARABU
NJIA YA ELIMU NA USTAARABU
Author :
Publisher :
(0 Kura)
(0 Kura)
NJIA YA ELIMU NA USTAARABU
Hapana shaka kuwa Njia ya Furaha hapana budi kupita katika njia za elimu na ustaarabu, haiwezekani kwa hali yoyote kupita katika mabonde ya ujinga, na haipatikani dini wala fikra ambayo imenyanyua hadhi ya wanazuoni na
kuheshimu miamala yao na kuhimiza kutafuta elimu na kuitumia akili na kulingania katika mazingatio na kufikiria kama mfano wa dini ya Uislamu aliokuja nao Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ambae alijenga ustaarabu mkubwa ulioenea mashariki ya ardhi na magharibi yake.
Kwa hali hiyo kutumwa kwake Swala Llahu ‘alayhi wasallam kunahesabiwa kuwa ni mapinduzi ya kweli ya kielimu katika mazingira ambayo roho ya kielimu imeyazoea, Kwa hiyo Uislamu ukaja ili elimu ianze, na dunia ing’are
kwa nuru ya uongofu wa Mwenyezi Mungu, Akasema Aliyetukuka: {Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?} [5:50].