SHAHIDI KWAAJILI YA UBINADAMU
SHAHIDI KWAAJILI YA UBINADAMU
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publish number :
Toleo la kwanza
Publish location :
Dar es Salaam, Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
SHAHIDI KWAAJILI YA UBINADAMU
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiingereza kwa jina la: The Martyr For Mankind. Sisi tumekiita: Shahidi Kwa Ajili Ya Ubinadamu. Kitabu hiki kinazungumzia masaibu yaliyotukia Karbala. Masaibu ya Karbala ni maarufu sana. Kila mwaka unapofika mwezi wa Muharram, Waislamu duniani kote hufanya majlisi (mikusanyiko) kwa ajili ya kuomboleza masaibu yaliyompata Imam Husain (as) - mtoto wa Imam Ali (as) na Fatima (as) ambaye ni mjukuu halisi wa Mtukufu Mtume (saww). Kwa hakika masaibu haya yanazidi kuwa maarufu kadiri miaka inavyozidi kwenda. Waislamu wanazidi kuathiriwa mno na masaibu haya, na kuwa na hamu ya kutaka kujua zaidi masaibu haya yaliyompata mjukuu huyu wa Mtukufu Mtume (saww) yametokana na nini na yamesababishwa na nini hasa. Kama ilivyo vitabu vyingi vinavyohusu masuala ya dini vimeandikwa kwa lugha za kigeni, vivyo hivyo maelezo ya masaibu haya mengi yamo kwenye lugha za kigeni, na hivyo Waislamu wengi wazungumzaji wa Kiswahili wamekuwa hawazipati habari hizi moja kwa moja kupitia kwenye vitabu, ila kwa kuhudhuria majlisi. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Mganga B. Mnuve kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.