Swali_la_Sheikh_Abdullah_Saleh_al_Farsy
Swali_la_Sheikh_Abdullah_Saleh_al_Farsy
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
1999
Publish location :
Tanzania Dar es salaam
(0 Kura)
(0 Kura)
Swali_la_Sheikh_Abdullah_Saleh_al_Farsy
Tunayo furaha kuchapisha barua kutoka kwa Mwanachuoni mashuhuri na maarufu katika Afrika Mashariki Sheikh Abdullah Saleh al-Farsy, pia tunachapisha jibu la Imam Muhammad Husain Kashiful Ghitaa, mwanachuoni kutoka Iraq anayetambulika kimataifa. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Sayyid Mohammad Radha, mwanae Sayyid Muhammad Mehdi Shushhtary mwenye asili ya Zanzibar na ambaye wakati huu anaishi Iran, kwa kuongezea makala zinazowatambulisha Sheikh Abdullah Saleh al-Farsy na Imam Muhammad Husain Kashiful Ghitaa, ambao wanajulikana vema ulimwenguni kote. Hii ni kwa manufaa ya kizazi kipya ambao pengine watakuwa hawajui wao. Pia tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Masheikh Haroun R. Pingili na Musabbah Shaban, kwa msaada wao wa kupitia kitabu hiki na kutoa maoni yao ambayo yamewezesha kufanikisha kitabu chote.