Uongozi wa Kidini MaeleKezo na UteKelezaji wa KijaMii

Uongozi wa Kidini MaeleKezo na UteKelezaji wa KijaMii

Uongozi wa Kidini MaeleKezo na UteKelezaji wa KijaMii

Publication year :

2014

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Uongozi wa Kidini MaeleKezo na UteKelezaji wa KijaMii

Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, al-Qiyadutu ‘l-Diniyyah, al-Khitab wa ‘l-Ada’u‘-Ijtima’i. Sisi tumekiita, Uongozi wa Kidini: Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii.
Kitabu hiki kinazungumzia uongozi, hususan uongozi wa kidini. Uongozi katika shughuli yoyote ni muhimu sana ili kufanikisha malengo yake na kufikia ufanisi wa hali ya juu na kuweza kuwanufaisha wale wanaoongozwa. Katika kitabu hiki mwandishi anajaribu kuelezea umuhimu wa uongozi na viongozi katika jumuiya na taasisi zetu za Kiislamu, hali ya uongozi wa zamani na uongozi mzuri unaotakikana kwa sasa bila ya kuvuka mipaka ya dini. Na hii ana maana ya kufuata kanuni na maadili ya Uislamu kama ilivyoainishwa katika Qur’ani Tukufu na Sunna.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na sayansi na tekinolojia, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu.
Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Abdulkarim Juma Nkusui kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kwa lugha ya Kiswahili; pia wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin.