WAKFU, SADAKA NA HUDUMA KATIKA UISLAMU

WAKFU, SADAKA NA HUDUMA KATIKA UISLAMU

WAKFU, SADAKA NA HUDUMA KATIKA UISLAMU

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

WAKFU, SADAKA NA HUDUMA KATIKA UISLAMU

Wakfu ni aina maalumu ya sadaka yenye kuendelea na inayodhihirisha lin-aloelezea huruma, upendo wa kindugu na mahabba kwa viumbe kwa ajili ya Muum-ba wao. Hii inahusisha kujitolea mali maalumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kwa maneno mengine, ina maana ya ku-zuia moja kwa moja tamlik na tamalluk1ya umilikaji wake na kuitunza na kuilinda kwa faida ya jambo la heri lililokusudiwa. Lengo lake ni kupata radhi za Mwenye-zi Mungu kwa kuitoa kwa heri kuwapa masikini, na kuwahurumia kwa huruma na upendo wa kweli, kutoa mali - hata maisha inapohitajika – kwa ajili ya Mwe-nyezi Mungu ni amri ya Mwenyezi Mungu ambayo Waislamu wote wanalazimika kuitii kwa sababu ni sharti la ukamilifu wa imani. Imeamriwa ndani ya Qur’an Tukufu Kuwa