waulize_wanaofahamu

waulize_wanaofahamu

waulize_wanaofahamu

Publication year :

2001

Publish location :

Dar es salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

waulize_wanaofahamu

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho Fas'alu Ahladh-Dhikr kilichoandikwa na Shaikh Muhammad Tijani Samawi wa Tunisia. Ndani ya Kitabu hiki ameelezea mkusanyiko wa itikadi za Kiislamu kwa namna zilivyo ndani ya Qur'an na Sunna Tukufu ya Mtume (s.a.w.w). Kitabu hiki ni kama vile vya mwanzo, nacho kimepata umaarufu hasa kutokana na jinsi mwandishi alivyozichambua itikadi hizo kwa mujibu wa mtazamo wa Sunni na Shia, kisha akayabainisha maeneo wanayohitilafiana. Kwa mara nyingine tena mimi binafsi sikusita kumuomba Shaikh Musabah Shaban Mapinda kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake ya lugha ya Kiarabu. Sababu iliyoifanya Tasisi zetu isimamie kazi hii ni kama zile za mwanzo, ambayo inatokana na maombi ya Maulamaa wengi katika Afrika Mashariki kututaka tukifasiri kitabu hiki kiingie kwenye lugha ya Kiswahili. Namshukuru Shaikh Musabah kwa kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja. Nimeiangalia pamoja naye tafsiri hii kwa makini kuhakikisha kuwa maudhui yake ya asili hayakupotoshwa katika lugha ya Kiswahili. Shaikh Tijani Samawi ameandika vitabu vifuatavyo, Thummah-Tadaytu, Li Akuna Ma'as-Sadiqin na Fa'salu Ahladh-Dhikr, na Sheikh Musabah Shaban Mapinda amezitafsiri vitabu zote tatu za mwandishi huyu chini ya Tasisi ya Ahlul-Bayt (a.s) Assembly of Tanzania (ABATA) kwa lugha ya kiswahili viitwavyo Hatimaye Nimeongoka, Hi Niwe Pamoja Na Wakweli na Waulizeni Wanaofahamu, vilivyo pangwa katika kompyuta na Ahlul-Bayt (a.s)Assembly of Tanzania na kuchpishwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tena kwani vitabu zetu "Hatimaye Nimeongoka na Hi Niwe Pamoja Na Wakweli "kimependwa mno na wasomaji na hivyo kutupa ari ya kuchapisha hiki ulichonacho mkononi. Ushahidi wa kupendwa kwa kitabu hicho ni shukurani na pongezi tunazozipokea toka kwa wasomaji kwa namna mbalimbali ikiwemo kutuandikia barua n.k. BILAL na ABATA zinatoa shukurani kwa mfasiri na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine katika uchapishaji wa kitabu hiki. Wa Ma Tawfeeqi IlIa Billah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Dar-es-salaam 29th Zilqaadah, 1422 13th Feb, 2001.