HISTORIA FUPI YA FATIMA ZAHRAA (A.S)
HISTORIA FUPI YA FATIMA ZAHRAA (A.S)
0 Vote
136 View
HISTORIA FUPI YA FATIMA ZAHRAA (A.S) JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S). Jina lakeniFatima binti wa Mohammad (s.a.w) bin abdallah bin abdul mutwalib. MAMA YAKE (A.S). Mama yake ni Khadija binti Khuwailid. KUNIA YAKE (A.S). Kunia yake ni 1- ummu abiiha. 2- Ummul hassanaini. 3- Ummul aimmah. 4- Ummur rihaanataini, na mengineyo. JINA LAKE MASHUHURI (A.S). Jina lakemashuhuri ni 1- Zahraa. 2- Al batuul.3- Swiddiiqah. 4- Mubaraakah. 5- Twahira. 6- Zakiyyah. 7- Radhiyyah. 8- Mardhiyyah. 9- Al muhaddathah, na mengineyo. TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S). Fatima Zahraa alizaliwa tarehe 20 jumadal Aakhir mwaka wa tano wa utume kutokana na kauli iliyo mashuhuri kwa mashia, na kuna kauli zingine zisemazo kuwa alizaliwa katika tarehe tofauti na hiyo. MAHALA ALIPO ZALIWA (A.S). Alizaliwa katika mji mtukuu wa makka. KUOLEWA KWAKE (A.S). Aliolewa na Amirul muuminina Ally bin abii twalib (a.s) WATOTO WAKE (A.S) Ali ruzukiwa watoto wafuatao: 1- Hassan (a.s) 2- Hussein (a.s) 3- Zainabul kubraa. 4- Zainabu As-sughraa. NEMBO YA PETE YAKE (A.S). Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo: (Aminal mutawakkiluun). MTUMISHI WKE (A.S). Mtumishi wake alikuwa akiitwa Fidhwah. UMRI WAKE. Ali ishi kwa muda wa miaka 18 kutokana na kauli iliyo mashuhuri. Na kuna kauli zingine tofauti na hiyo. KUFARIKI KWAKE. Alifariki Dunia tarehe 3 jamaadal Aakhir mwaka wa 11 hijiria, na riwaya nyingine inasema kuwa alifariki tarehe13 jamaadul ulaa, na kuna kauli nyingine tofauti na hizo. SEHEMU ALIPO ZIKIWA. Alizikwa katika mji wa madinatul munawwarah, na kuna tofauti kuhusiana na sehemu ya kaburi lake. Kwa ufafanuzi zaidi rejea katika kitabu Buharul an’waar, juzu ya 39, kwa wenye kufahamu lugha ya kiarabu. http://www.al-shia.org