HISTORIA FUPI YA IMAM HASSAN MUJTABA (A.S)
HISTORIA FUPI YA IMAM HASSAN MUJTABA (A.S)
0 Vote
137 View
HISTORIA FUPI YA IMAM HASSAN MUJTABA (A.S) JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S) Jina lake ni Hassan bin Ally bin abi twalib bin Abdul mutwalib. MAMA YAKE (A.S). Mama yake ni Fatima Zahraa binti wa Mtume (s.a.w). KUNIYA YAKE (A.S) NI. Abu mohammad. JINA LAKE MASHUHURI (A.S). 1- Attaqii. 2- Azzakii. 3- Assibtwi. 4- Atwayyib. 5- Assayyid. 6- Al walii. Na mengineyo. TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S) Alizaliwa tarehe 15 mwezi wa Ramadhani mwaka 3 hijiria, na hii ndio tarehe iliyo mashuhuri, na inasemekana ya kuwa alizaliwa mwaka wa 2 hijiria. SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S). Alizaliwa katika mji wa madinatul munawwarah. VITA VYAKE (A.S) Alishiriki katika ukombozi wa nchi za afrika na miji ya faris kati ya mwaka 25- 30 hijiria, na alishiriki katika vita vyote vya baba yake Ally bin abii twalib (a.s) kama, Jamal, Swifin, na Nehrawaan. WAKEZE (A.S) 1-ummu bashiir binti abi mas’uud al khazrajiyyah. 2- Khawla binti mandhuur al fazariyyah. 3- Ummu Is’haaq binti Twalha Attamiimiy. 4- Juu’da bintil ash-ath. WATOTO WAKE (A.S) 1- Zaidi bin Hassan. 2- Hassan bin Hassan. 3- Amru. 4- Qaasim. 5- Abdallah. 6- Abdur rahman. 7- Hussein bin Hassan. 8- Twalha. 9- ummul Hassan. 10- ummul Hussein 11- Fatima binti Ummu Is’haaq. 12- Ummu Abdallah. 13- Fatima bintil Hassan 14- Ummu Salamah binti Hassan. 15- Ruqayya binti hassan, na wengineo. NEMBO YA PETE YAKE. Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo, (Al izzatu lillahi wahdahu), na inasemekana kuwa kuna nembo nyingine tofauti na hii. UMRI WAKE (A.S). Ali shi kwa muda wa miaka 47. MUDA WA UIMAMU WAKE (A.S). Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 10. WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S). Muawia bin abii sufyaan. TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S). Alikufa shahidi tarehe 6 mwezi wa Safar mwaka 49 hijiria, na inasemekana alifariki tarehe 28 safar mwaka 50 hijiria. SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI (A.S). Alifia katika mji wa Madinatul munawwarah. SABABU YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S). Alilishwa sumu na muawia kupitia mkewe alie kuwa akiitwa Juudah bintil ash’ath. SEHEMU ALIPO ZIKIWA (a.s). Alizikwa kwenye makaburi ya baqii yaliyoko kwenye mji wa Madintul munawwarah. Kwa ufafanuzi zaidi rejea kitabu Buharul an’waar juzu ya 39-40 kwa wenye kufahamu lugha ya kiarabu. http://www.al-shia.org