Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Muhammad (a.s.)

Wasifu mfupi wa Imam Ali bin  Muhammad (a.s.)

Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Muhammad (a.s.)

Publication year :

2012

Number of volumes :

1000

Publish number :

Toleo la Kwanza

Publish location :

Dar es Salaam - Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Muhammad (a.s.)

Hatimaye, Kwa Rehema za Allah, nimekamilisha kuandika wasifu huu mfupi wa Imamu wetu wa kumi, Imam Ali Naqi (a.s.) kwa ajili ya wasomaji wale ambao wanahitaji kupata mukhtasari wa maisha ya Imam huyu aliyeteuliwa kimungu. Kuna taarifa nyingi mno juu maisha ya Imam wetu wa kumi kiasi kwamba katika hatua za mwanzo nilikuwa sina dalili ya wapi pa kuanzia na wapi pa kumalizia jukumu hili la kutisha ambalo nimekubali kulifanya kwa niaba ya Bilal Muslim Mission of Tanzania. Jinsi ninavyozidi kufikiria kuhusu mradi huu, ndivyo ninavyozidi kuhisi kuvunjika moyo, mpaka wakati nilipogundua kwamba kulikuwepo na watu wachache waliosoma wasifu fupi nilizoandika juu ya Maimam wengine, na ambao walikuwa wanaulizia kutoka Bilal Muslim Mission wapewe maelezo ya kwa nini sikuandika juu ya maisha ya Maimam wetu wa kumi, wa kumi na moja na wa kumi na mbili. Kuuliza huku kwa mara nyingine tena kulinipa moyo zaidi kujikusanya na kutumia nguvu zangu kwenye jukumu hili ambalo halijakamilika. Matokeo ya juhudi hii ni mukhtasari huu mfupi unaolezea maisha ya Imam wa kumi, Hazrat Ali Naqi (a.s.). Kila mara ninapopitia kazi hii wakati ikiwa bado katika muundo wa muswada, nilikuwa naona kwamba bado ilikuwa haifai kuchapishwa kwa vile haikufikia hata mambo muhimu ya msingi ya haiba ya mtu huyu maarufu. Niliishia kwa kufanya marekebisho mengi mno. Hatimaye, nilifikia hitimisho kwamba kama nitafuata silka yangu, kamwe kazi hii haitamalizika. Kwa hiyo sasa tunayo kazi hii fupi kwa ajili ya wasomaji wangu. Maombi yangu kwa Muumba ni kwamba Anisamehe kwa mapungufu ambayo huenda yamebakia bila kuonekana katika kitabu hiki. Nachukua fursa hii kuwashukuru wote wale ambao kwa njia moja au nyingine wamenisaidia katika juhudi zangu za kufanya na kukamilisha jukumu hili. Shukurani zangu maalumu za moyoni ni kwa ajili ya Mzee Fidahusein Abdullah Hameer, Mchapishaji, ambaye alivumilia kukawia kwangu na huku mara kwa mara akinikumbusha jukumu langu la kukamisha kazi hii.