Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Musa (a.S.)
Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Musa (a.S.)
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2012
Number of volumes :
1000
Publish number :
Toleo la Kwanza
Publish location :
DAR ES SALAAM - TANZANIA
(0 Kura)
(0 Kura)
Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Musa (a.S.)
Mwishoni mwa miaka za 50 na mapema miaka za 60, wakati nilipokuwa mwanafunzi wa Madrasa katika shule ya Faize Zanzibar, kulikuwa hakuna somo kama la Historia ya Kiislamu katika mitaala ya Madrasa. Kwa hiyo, wakati nilipojiunga na kikosi cha kufundisha cha Husseini Madrasah mjini Dar es Salaam, Tanzania mapema katika miaka za 80, na hatimaye nikateuliwa kufundisha somo la Historia ya Kiislamu, nilichanganyikiwa nikiwa sijui ni kitu gani nifundishe. Sio tu kwamba kulikuwa hakuna mtaala kwa ajili ya somo hili. Bali, wajibu wangu mkubwa ulikuwa ni upeo wa mtaala wenyewe. Kwani kwenye kiini cha Mtaala wa Historia ya Kiislamu ilikuwa kujifunza maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale MASOOMIN kumi na tatu wengine ambao wanaotokana na kizazi chake. Kwa mtazamo wangu, mbali na kitabu bora cha Yusuf Laljee KNOW YOUR ISLAM (UJUE UISLAMU WAKO), kulikuwa hakuna kita-bu kingine rahisi bali hata maandiko ya kielimu ambayo yanaweza kutumiwa kwa kujitosheleza kwa wote, walimu na wanafunzi kwa usawa. Hata hivyo, sehemu ya historia ya maisha ya MASOOMIN ilikuwa sio kamili katika kitabu KNOW YOUR ISLAM. Kuanzia siku hizo, nilihisi haja ya kukusanya kwa ufupi mukhtasari wa kufundishia juu ya maisha ya Maimam wetu kumi na mbili (a.s.) pamoja na malengo mawili akilini. Kwanza, kuangalia katika maeneo yote yale ya habari, bila kuacha taarifa za kihistoria, ambazo zitamuwezesha mwanafunzi kuelewa hali changamani ambayo kwayo Maimam wetu wameishi na kutekeleza majukumu yao kama wateule viongozi wa kiungu wa ulimwengu. Pili, kuwasilisha taarifa hii katika mtindo ambao una kiini chake cha masilahi, hali kadhalika na uwezo ulio sawa wa walimu na wanafunzi. Niliona jukumu hili ni rahisi kuingia akilini lakini gumu sana kulitekeleza. Ni wazi kwamba, ningeweza kukamilisha kidogo katika eneo hili mpaka wakati nilipohamia Marekani. Kwa bahati mbaya au nzuri, katika Husseini Madrasah wa New York, kwa mara nyingine tena niliteuliwa kufundisha Historia ya Kiislamu. Kwa sababu ambazo sihitaji kuzieleza hapa, niliona jukumu hili la kutisha mno kuliko ilivyokuwa katika Afrika. Kwa bahati nzuri, katika wakati huu mgumu wakati nikiwa napapasa gizani nikitafuta maandiko bora ya kufundishia kwa ajili ya darasa langu, niliteuliwa na by Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Mhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, kuandika vijitabu vya kufundishia vinavyohusisha maisha ya Maimam wetu 12 (a.s.) kwa ajili ya Masomo kwa Njia ya Posta yanayoendeshwa na Bilal Mission. Kwangu mimi hii ilikuwa neema ya Allah iliyoletwa katika njia mbili: Kwanza, uteuzi huu ulinipa moyo na imani ambayo nimeikosa mpaka sasa. Sasa ninao msaada wa mmoja wa mwanachuoni maarufu wa Shia wa zama yetu hii – Sayyid Saeed Akhtar Rizvi. Pili, sitakuwa na wasiwasi kuhusu kutafuta mfadhili kwa ajili ya uchapishaji na usambazaji wa maandishi yangu; Bilal Muslim Mission of Tanzania italifanya hilo. Kwa hiyo, kijitabu hiki na vyingine vitakavyokuja ni matokeo ya ari na msaada kamili wa Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, utawala wa Bilal Muslim Mission of Tanzania mwenyekiti wake wa zamani Al-haj Fidahusein Abdullah Hameer. Yote, mada, hali kadhalika na mtindo wa kijitabu hiki (na vingine vifuatavyo) vimefanywa vyepesi kueleweka, ili kuafikiana na ushauri wa Maulana Sayyid Saeed Akhtar kwamba “Lazima tuzingatie kwamba vijitabu hivi vya masomo vimekusudiwa kwa vijana na sio kwa wanachuoni.” Yote yamesemwa na kufanywa, licha ya tahadhari ya hali ya juu zilizochukuliwa ili kukifanya kijitabu hiki kuondokana na kasoro na makosa mengine. Hata hivyo, kama baadhi yamebakia bila kusahihishwa, mimi ndiye muwajibikaji. Allah anisamehe kwa makosa haya ambayo hayakukusudiwa na awalipe wale wote ambao wamenisaidia kwa njia moja au nyingine katika kuandika, uchapishaji na usambazaji wa kijiatabu hiki.