Wasifu mfupi wa Imam Husayn (a.s.)

Wasifu mfupi wa Imam Husayn (a.s.)

Wasifu mfupi wa Imam Husayn (a.s.)

Interpreter :

MUHAMMAD S. KANGU

Publication year :

2012

Number of volumes :

1000

Publish number :

Toleo la Kwanza

Publish location :

DAR ES SALAAM - TANZANIA

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Wasifu mfupi wa Imam Husayn (a.s.)

Haya yalikuwa ni matakwa ya Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi kwa miaka kadhaa sasa, kujumuisha wasifa za Maasumeen 14 katika Masomo yetu ya Kimataifa kwa njia ya Posta, lakini kutokana na shughuli zake kuwa nyingi ulimwenguni pote ilimzuiya kulitekeleza jukumu hili. Bilal Muslim Mission of Tanzania inamshukuru sana Dr. Mohammed Raza M. Dungersi wa New York ambaye amejitolewa kulitekeleza jukumu hili gumu na la kutisha. Hakuna mwanahistoria au mwandishi yoyote, kwa umahiri wowote atakaokuwa nao, awezaye kutoa picha ya kweli ya maisha ya Maasumeen (a.s.). Hata hivyo, tunampongeza Dr. Dungersi kwa juhudi hii kubwa na kumuomba Allah amlipe malipo mema hapa duniani na kesho Akhera. Maisha ya watu wa kubwa hutukumbusha jinsi ya kufanya maisha yetu kuwa na msukumo. Historia ya watu wakubwa ni chemchemi ya elimu, imani na ari amabyo kamwe haitakauka. Maisha ya watu hawa ni kama nyumba za mwanga, ambazo huondoa giza na kuonesha njia iliyonyooka kwa wasafiri wanaotafuta elimu, maisha bora na huduma kwa wanadamu. Lau kama watu hawa wakubwa wasingeacha nyayo juu ya mchanga wa zama, ulimwengu ungekuwa unapapasa gizani na ungeangukia kuwa mawindo kwenye ukataji tamaa wakati ambapo unapambana na nguvu na akili zisizoonekana. Hili ni chapisho la tatu katika mfululizo wa mradi huu mkubwa ambao chini ya mfululizo huu wa vijitabu hivi linakwenda kuchapishwa. Dr. Dungersi tayari amakamilisha wasifu wa Maimam wetu wanne wa mwanzo.