Al-Wahda umoja ya waislamu

Al-Wahda umoja ya waislamu

Al-Wahda umoja ya waislamu

Publication year :

2006

Publish location :

Dar es salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Al-Wahda umoja ya waislamu

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiaarabu kilichoandikwa na Mwanachuoni: Sayyid Murtadha Al- Ridhwi. Kitabu hiki kinahusu umoja wa Waislamu, mada ambayo ni muhimu sana tokea zamani, na ambayo umuhimu wake umezidi sana katika zama hii tuliyo nayo sasa. Maadui wa Uislamu wametangaza wazi wazi kwamba: sasa baada ya kuusambaratisha ukomunisti, adui yetu aliyebaki ni Uislamu na Waislamu. na wote tumeona walivyofanya na wanavyoendelea kufanya katika nchi za Kiislamu, nenda Afghanistan angalia walivyofanya, nenda Iraq angalia walivyofanya, nenda Pakistan angalia wanavyo wagombanisha Waislamu kule kwa kuzikuza tofauti za Madhehebu. Sasa hivi wameiandama Iran, kisa, Iran wanataka kutengeneza nishati ya nyukilia kwa matumizi yao ya viwanda na matumizi mengine ya kawaida (sio kwa ajili ya silaha), lakini wimbo unaoimbwa na maadui hawa ni kwamba Iran wanataka kutengeneza silaha za maangamizi. Ajabu ni kwamba wamesahau silaha za maangamizi walizonazo wao na ambazo wamezitumia huko Hiroshima Japan na kuteketeza maelfu ya watu, na athari yake inaendelea mpaka leo. Ukweli ni kwamba Maadui hawa hawataki kuona Waislamu wanaendelea katika nyanja yoyote ile, kwa hiyo wanatumia kila hitilafu tulizo nazo ili kutusambaratisha. Na kwa kiasi fulani wamefanikiwa, na kama hatutanabahi basi hali itakuwa mbaya zaidi upande wetu Waislamu, ni muhimu hilo kulitambua. Mwandishi wa kitabu hiki amekusanya maoni ya wanachuoni wakubwa wa Sunni na Shia, na wote wamesisitizia juu ya umoja wa Waisalamu bila kujali Madhehebu zao. Ili kuweza kukabiliana na maadui hawa, hatuna budi sisi kufuata ushauri wao.