Changamoto, Mafanikio, na Maisha ya Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Changamoto, Mafanikio, na Maisha ya Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Changamoto, Mafanikio, na Maisha ya Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Interpreter :

Salman Shou

Publication year :

2022

Publish location :

Canada

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Changamoto, Mafanikio, na Maisha ya Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Bila ya Rehema Neema ya Mungu (tawfiq) haingewezekana mtu kukamilisha kwa namna isiyo ya kawaida
kwa mtu ambaye amehamia kwenye nchi ya kigeni, bara tofauti,kuwa katika lugha na utamaduni usiozoeleka kwake, akiwa na nia ya kueneza ujumbe wa Uislamu na madhehebu ya Shia, bila ya mali ya kutosha, kwa kweli ni mafanikio makubwa sana. Hii ni hadithi ya baba yangu, ‘Allāmah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (Mwenyezi Mungu Muweza wa Yote na ainue hadhi yake).
Marehemu Ayatullah Shaykh Muhammad Mahdi al-Asifi aliandika vizuri sana kwa kifupi mafanikio ya baba yangu kwa kuyahusisha na maisha ya Mtume Musa (a): “Alikwenda safari ya kutafuta kijinga cha moto lakini alirudi na kitu gani? Alirudi na nuru ya unabii. Musa alikwenda kutafuta nini, na akarudi na kitu gani?
Hiyo inajulikana kama Rehema na Neema ya Mungu (tawfiq).”1 Kuandika wasifu wa mtu ambaye maisha yake ya kiutendaji yalidumu nusu karne akiwa amezuru mabara manne sio kazi rahisi. Kwa bahati njema, marehemu baba yangu alikwisha anza mlolongo huu alipoandika kitabu kiitwacho Shajarah-e Ṭayyibah, kwa lugha ya Kiurdu, kuhusu maulama watano wa kutoka miongoni mwa wahenga wetu wa karibu, akiishia na babu yangu marehemu Maulana Ḥakīm Sayyid Abul Ḥasan Rizvi