Falsafa ya dini
Falsafa ya dini
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2010
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Falsafa ya dini
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Philosophy of Religion, kilichoandikwa na Sayyid Jawad Naqvi. Sisi tumekiita Falsafa ya Dini. Kitabu hiki huelezea kwa ujumla falsafa na hekima ya dini na jinsi ya kuifuata dini pamoja na changamoto zake. Mwandishi ameandika kitabu hiki kwa kuwalenga Waislamu wa Pakistan na India ili kuwaasa kwa ajili ya masaibu wanayoyapata mikononi mwa mabeberu. Lakini hali hii ipo pia katika nchi nyingine za Kiislamu, kama vile Iraq, Afghanistan, Palestina, na inanyemelea nchi nyingine za Kiislamu na kwa Waislamu popote wanapoishi ulimwenguni. Hivyo, ni jukumu la kila Mwislamu popote alipo kuchukua tahadhari na kuungana na Waislamu wote ulimwenguni kuukataa unyanyasaji huu unaofanyiwa Waislamu. Waswahili wanasema: “Ukimwona mwenzako ananyolewa, wewe tia maji kichwa chako.” Lakini pia tunajifunza kutokana na makosa ya wenzetu. Leo hii ni Pakistan, kesho ni Kenya, na keshokutwa ni Tanzania. Hili ni somo la kuzingatiwa. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa utandawazi ambapo dunia imekuwa kama kijiji. Hakuna linalotokea upande mwingine wa dunia bila kuugusa upande mwingine. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.