FITINA ZA WAHHABI ZAFICHULIWA

FITINA ZA WAHHABI  ZAFICHULIWA

FITINA ZA WAHHABI ZAFICHULIWA

Interpreter :

Mohammad Said Kanju

Publication year :

2005

Number of volumes :

5000

Publish number :

Toleo ya Saba

Publish location :

Dar es Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

FITINA ZA WAHHABI ZAFICHULIWA

Tunamshukuru Allah (s.w.t.), kwa Baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Watukufu Ahlul-Bait (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha toleo la saba la kitabu hiki “Fitina Za Wahhabi Zafichuliwa.” Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya moja ya ma’andishi ya Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a.). Kitabu hiki kimekuwa maarufu katika ulimwengu wa Ki-Islamu na kilitafsiriwa na kuchapishwa na Taasisi mbali mbali kwa lugha ya Ki-Ingereza, Ki-Urdu na Kiarabu. Sababu iliyoifanya Bilal Muslim Mission isimamie kazi hii ni kama zile za mwanzo, ambayo inatokana na maombi ya watu wengi kutoka Afrika ya Mashriki kututaka tuchapishe Kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili. Hii ilitufanya tutafsiri na kuchapish kitabu hiki ili watu wazungumzao kiswahili waweze kuelewa na kufahamu zaidi juu ya suala hili na fitina hizi za maadui wa Uislamu. Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa mfasiri wa kitabu hiki Ndugu Dr. Mohammad Kanju na wale wote ambao kwa juhudi zao toleo hili la saba la kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi mwao na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine katika kazi zetu za Tabligh. Tunamuomba Allah (s.w.t.) awal-ipe malipo mema hapa Duniani na baadaye huko, Akhera.