Jawabu kwa wapinga Maulidi
Jawabu kwa wapinga Maulidi
Author :
(0 Kura)
(0 Kura)
Jawabu kwa wapinga Maulidi
KIISLAMU. SHEREHE ZA MAULIDI NI ZENYE KUPEWA KIPAU MBELE SANA NA WATU WA MUAMBAO WA AFRIKA YA MASHARIKI, SABABU KUU ILIYO WAFANYA WAO KUWA NA SHAUKU YA MAULIDI KILA IFIKAPO MFUNGUO SITA, NI KULE KUWA WAO, NI WAISLAMU WENYE MAPENZI NA MTUME WAO. KATIKA ZAMA ZA MIAKA KAMA ISHIRINI AU KUMI NA TANO ILIYOPITA, KULIANZA KUINGIA VURUGU LA BAADHI YA WAISLAMU WENYE SIASA KALI, LILILOWATANGAZIA WENGINE UHARAMU WA MAULIDI, HAIDHURU KATIKA USEMI WAO HUO, HUWA WANATOA DALILI MBALI MBALI, LAKINI WAKATI MWENGINE DALILI ZAO HUWA HAZIKUBALIKI KIMANTIKI. KITABU HIKI KILICHOKO MIKONONI MWENU NI KITABU KILICHO KUSANYA JUMLA YA MAKALA MABALI MBALI ZILIZITAYARISHWA NA SHEIKH ABDILLAHI NAASIR, KWA AJILI YA KUJIBU HOJA MBALI MBALI ZA WAPINGAJI WA MAULIDI. NA MIMI KWA UPANDE WANGU NIMEAMUA KUUWEKA UTANGULIZI HUU, ILI TU NIWEZE KUTOA MTAZAMO WA SUALA HILI LILIVYO INGAWAJE NI KWA UFUPI KABISA. NINATARAJI WAISLAMU WENZETU WATAFAIDIKA NA MAELEZO HAYA, NA WATALITUMIA JICHO LA KUTAFAKARI KATIKA KUYAANGAZA YALIOMO NDANI YA MAKALA HIZI. NINAMUOMBA MOLA MTUKUFU ATUNUSURU NA SHARI ZA UJINGA WETU, NA ATUPE UFUNUO WA ELIMU ITOKAYO MBINGUNI. KWANI YEYE TU NDIYE MJUZI NA KIONGOZI WA WACHA MUNGU. AAMIN YAA RABBAL AALAMIIN.