Jihadi
Jihadi
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2014
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Jihadi
K itabu ulichonacho mikononi mwako kimetarjumiwa kutoka lugha ya Kiarabu na kuitwa, Jihadi. Kitabu hiki kimeandikwa na Ustadh Murtadha Mutahhari.
Jihad maana yake ni vita vitakatifu. Katika istilahi ya Kiislamu, Jihadi ni vita ambavyo hupiganwa kwa ajili ya kuitetea na kuilinda dini ya Mwenyezi Mungu. Jihadi ina taratibu na sheria zake, haipiganwi kiholela, kwani kwanza lazima ipatikane ruhusa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) au Imam wa zama au naibu wake.
Mwandishi katika kitabu hiki ameainisha masharti yote na mambo ya kuzingatiwa katika vita hivi vitakataifu na adabu zake. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo tunashuhudia vita kutoka kila mahali ulimwenguni na vingine vimepewa jina la Jihadi kinyume na masharti yaliyowekwa na dini ya Kiislamu.
Hivyo, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kutoka Kiarabu. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin kisha Amin