JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

Interpreter :

Hemedi Lubumba

Publish number :

Toleo la kwanza

Publish location :

Dar es Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Jawaahiru ‘l-Hikmah li ‘sh-Shabaab ambacho tumekifupisha na kukiita, Johari za Hekima kwa Vijana. Kwa hakika kitabu hiki kinazungumzia maadili ya vijana kwa mtazamo wa Kiislamu. Kama tujuavyo, Uislamu ni dini na mfumo wa maisha, kwa hiyo, haukuacha chochote kinachomhusu mwanadamu katika maisha yake ya hapa duniani na ya kesho Akhera. Mwandishi wa kitabu hiki amejaribu kwa uwezo wake kuwakumbusha vijana juu ya wajibu wao katika jamii na kuwarejesha katika maadili mema. Na katika kuikamilisha kazi yake hii amerejea sana kwenye mafunzo ya Uislamu ambayo chimbuko lake ni Qur’ani na Sunna. Hivyo basi, huu ni mwongozo halisi kwa vijana unaolenga kuwaokoa katika harakati zao za maisha na hatimaye wawe ni wenye kufuzu kesho Akhera. Sisi tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo vijana wengi wamejitumbukiza katika mambo yenye kuangamiza maisha yao kwa kuacha utamaduni wao bora wa Kiislamu na kuiga tamaduni potofu, fasiki na fisadi za watu wa Magharibi (wazungu). Watu wenye busara huiga mambo mazuri na huwaachia wenyewe yale machafu, lakini kwa vijana wetu sivyo, wamepupia sana katika kuiga kama kima kila jambo karihifu la watu wa Magharibi. Hivyo kitabu hiki kitakuwa ni mwongozo mzuri kwa vijana wetu wa Kiislamu na hata wasio Waislamu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu ya dini ni ya jamii.