Kanuni za sharia za kiislamu
Kanuni za sharia za kiislamu
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2015
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Kanuni za sharia za kiislamu
K itabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahili ya kitabu cha Kiingereza kilichoandikwa na Mohammad Ali Shomali kiitwacho, Principles of Jurisprudence. Sisi tumekiita, Kanuni za Sharia za Kiislamu.
Uislamu ni dini na ni mfumo kamili wa maisha. Maana yake unahudumia roho na mwili. Kwa hiyo umeweka sheria na kanuni zenye kukidhi maisha ya hapa duniani na maisha ya kesho Akhera. Katika kitabu hiki mwandishi ameainisha na kuelezea baadhi ya kanuni na sheria ambazo kwazo mwanadamu anatakiwa azizingatie ili apate kuishi maisha bora na kufuzu kiroho ili akaishi maisha bora ya milele kesho Akhera.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, husasan wakati huu wa maendeleo makubwa ya kielimu ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, taasisi yetu ya al-Itrah imeamua ku- kichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake
yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera. Amin!